Kiongozi wa idara ya masayyid, Sayyid Hashim Shami amesema “Watumishi wa Ataba tukufu wamekamilisha kazi ya kusafisha haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kutandika mazulia, kupitia ratiba yao endelevu ya usafi na kubadilisha mazulia”.
Akaongeza kuwa “Kazi imehusisha utandikaji wa mazulia ya kifahari baada ya kumaliza usafi kisha wakapuliza marashi na kufukiza kwa manukato bora zaidi”.
Malalo tukufu husafishwa na kupuliziwa manukato wakati wote, ili kuweka harufu nzuri kwa mazuwaru wanaokuja sehemu hiyo takatifu kutoka kila kona ya dunia.













