Makamo rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya Sayyid Ahmadi Shakiri amesema “Watu wa Karbala wamezowea kuomboleza kifo cha mbora wa wanawake duniani (a.s) katika mji wa Najafu, ili kumpa pole Imamu Ali (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Maukibu ya kuomboleza hufanywa na watu wa Karbala kila mwaka kwa kushirikiana na Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Watu wa Karbala hufanya mawakibu za kuomboleza pamoja na majaalisi za kuwataja Ahlulbait (a.s) na kuhuisha elimu na utukufu wao.









