Makatibu wakuu wa Ataba tukufu: wamesisitiza umuhimu wa kudumisha mawasiliano, kubadilishana uzowefu na kutoa huduma bora kwa mazuwaru

Makatibu wakuu wa Ataba tukufu za Iraq, wamesisitiza umuhimu wa kudumisha mawasiliano na kubadilishana uzowefu kwenye sekta tofauti, ili kutoa huduma bora kwa mazuwaru.

Yamesemwa hayo katika kikao maalum cha makatibu wakuu wa Atabatu Alawiyya, Husseiniyya, Kadhimiyya, Askariyya na Abbasiyya, kilichofanywa ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini amesema “Kongamano limejikita katika kueleza umuhimu wa kudumisha mawasiliano baina ya Ataba tukufu na kubadilishana uzowefu kwenye sekta tofauti, kama vile afya, elimu, malezi, Dini, utamaduni na miradi mingine”.

Akaongeza kuwa “Kongamano limejadili njia bora ya kuhudumia mazuwaru”, akaeleza “Umuhimu wa nafasi ya Ataba tukufu katika kupokea mamilioni ya mazuwaru kipindi chote cha mwaka”.

Katibu mkuu wa Atabatu Alawiyya Sayyid Issa Khurasani amesema “Kongamano hili ni fursa muhimu ya kubadilishana fikra na kuimarisha ushirikiano baina ya Ataba, jambo ambalo linasaidia kuboresha huduma kwa mazuwaru watukufu, mambo mbalimbali yamejadiliwa”.

Katibu mkuu wa Atabatu Husseiniyya Sayyid Hassan Rashidi Al-Abaji amesema “Ataba tukufu ni taasisi za kijamii na kidini zinakazi kubwa katika taifa la Iraq kidini na kibinaadamu, kongamano la leo tumejadili mambo tunayoshirikiana, ambapo tunatakiwa kushikamana kwa ajili ya kupambana na changamoto na kuendana na maendeleo ya dunia”.

Akaongeza kuwa “Ataba tukufu zinamchango mkubwa wa kutoa misaada kwa ndugu zetu wapalestina, walebanon na wasiria, zinatoa misaada ya matibabu, chakula na malazi”, akasema kuwa “Kikao chochote cha viongozi wa Ataba katika mazingira haya ni sehemu ya uimara, kwani kinajenga Amani na utulivu kwa watu”.

Katibu mkuu wa Atabatu Kadhimiyya Dokta Haidari Shimri amesema “Kuna umuhimu wa Ataba tukufu kusaidia maeneo Fulani ya serikali ya Iraq, ili iweze kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa sharia na utaratibu”.

Akafafanua kazi kubwa inayofanywa na Atabatu Abbasiyya ya kupambana na magaidi wa Daesh katika baadhi ya mikoa ya Iraq, sambamba na kupokea wakimbizi kutoka Lebanon wakati wa mashambulizi ya waisrael, akapongeza juhudi ya kiongozi mkuu wa kisheria Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, katibu wake mkuu na watumishi wote kwa huduma nzuri wanayotoa kwa mazuwaru.

Naye katibu mkuu wa Atabatu Askariyya Dokta Naafi Jamiil Alkhuzai amesema “Ataba tukufu zinafanya juhudi kubwa ya kuimarisha ushirikiano na sekta tofauti katika jamii”, akasema kuwa “Kongamano limejikita katika kubadilishana fikra kwenye mambo mbalimbali, ili kuwa na maendeleo endelevu katika utendaji wa Ataba, sambamba na kujadili mambo yanayotuonganisha na kuweka mikakati ya utendaji”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: