Kwa matembezi ya kuomboleza.. chuo kikuu cha Al-Ameed kimeombeleza kifo cha Ummul-Banina (a.s)

Kitivo cha malezi ya msingi kwa wasichana kaika chuo kikuu cha Al-Ameed, kimefanya matembezi ya kuomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s) mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Muwakilishi wa mkuu wa kitivo Dokta Swabihi Kaabi amesema “Matembezi ya kuomboleza hufanywa kila mwaka mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ikiwa kama sehemu ya kumpa pole kwa kifo cha mama yake Ummul-Banina (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Chuo kikuu cha Al-Ameed huomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s) kutokana na utukufu wake katika historia ya Ahlulbait (a.s)”.

Akabainisha kuwa “Matembezi yanalenga kuimarisha misingi ya kidini kwa wanafunzi, kwa kuiga mwenendo mtukufu wa Ahlulbait (a.s) na kunufaika na nuru halisi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w)”.

Akasema kuwa “Chuo hufanya kumbukizi za matukio ya kidini likiwepo hili la kifo cha Ummul-Banina (a.s), kwa lengo la kujenga uwelewa wa Dini kwa wanafunzi na watumishi wa chuo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: