Kitengo cha mgahawa kimegawa zaidi ya sahani za chakula elfu 55 katika maombolezo ya Ummul-Banina (a.s)

Kitengo cha mgahawa katika Atabatu Abbasiyya kimegawa zaidi ya sahani za chakula elfu 55 kwa mazuwaru waliokuja Karbala kuomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s).

Rais wa kitengo Sayyid Aadil Hamami amesema “Watumishi wa kitengo cha mgahawa wamegawa chakula kwenye maeneo tofauti, kulingana na mahitaji ya mazuwaru katika siku tatu zilizopita za kuomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Kitengo kimegawa sahani za chakula 55,684 kwenye vituo viwili vilivyopo katika barabara inayoelekea kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na sehemu za ugawaji wa chakula za ndani ya haram tukufu”.

Atabatu Abbasiyya iliandaa ratiba maalum ya kuomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s) yenye vipengele vingi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: