Muwakilishi wa Marjaa-Dini mkuu katika mji wa Taju-Dini, Shekhe Saidi Jafari Twalali amesema “Natoa shukrani za dhati kwa Atabatu Abbasiyya na uongozi wake kwa kufanya hafla tukufu ya kuadhimisha mazazi ya Bibi Fatuma Zaharaa (a.s)”, akabainisha kuwa “Hafla imepata mahudhurio makubwa ya watu wa mji huu waliokuja kuadhimisha tukio hili tukufu”.
Mmoja wa watumishi wa idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Ataba tukufu, Shekhe Abdulhusein Twaaiy amesema “Katika kuadhimisha mazazi ya Bibi Zaharaa (a.s) tumekuja mkoani Waasit kushirikiana na waumini wa mji huu katika maadhimisho haya matukufu”.
Akaongeza kuwa “Katika hafla hiyo umeelezwa msimamo wa Bibi Fatuma Zaharaa (a.s), na kwa namna gani amekua kigezo chema katika subira na kujitolea kwake”.
Hafla imepambwa na mawaidha, maonyesho na kueleza nafasi yake katika uismalamu.
Hafla hiyo ni sehemu ya harakati za Atabatu Abbasiyya tukufu za kuhuisha matukio ya kidini sambamba na kuchukua mazingatio katika maisha ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s).








