Idara ya watoto na makuzi chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, imechapisha toleo la 181 la jarida la (Riyahaini) la kila mwezi.
Kiongozi wa idara hiyo Sayyid Hasanaini Faruuq amesema “Jarida linamilango mbalimbali yenye maudhui tofauti ambazo huandikwa kwa lugha nyepesi inayoendana na uelewa wa watoto”.
Akaongeza kuwa “Jarida linalenga kukuza uwezo wa watoto katika usomaji na kutafakari, ili kutengeneza kizazi cha watu wanaojitambua”.
Kitengo cha habari na utamaduni kupitia jarida la Riyahaini kinatengeneza mazingira mazuri ya kielimu kwa watoto.
