Idara ya Fatuma binti Asadi (a.s) ya masomo ya Qur’ani chini ya Atabatu Abbasiyya, imeanza kusajili washiriki wa semina ya (Yaasin) kwa wanawake.
Semina ni maalum kwa wasomaji wa Mimbari-Husseini katika mkoa wa Karbala, itadumu kwa miezi mitatu, inalenga kufundisha usomaji wa surat Yaasin kwa ufasaha na kuhifadhi sura fupi.
Zawadi nono zitatolewa kwa washindi watatu wa mwanzo kama ifuatavyo:
Mshindi wa kwanza: Dinari 200,000.
Mshindi wa pili: Dinari 150,000.
Mshindi wa tatu: Dinari 100,000.
Semina itafanyika Jumatano ya kila wiki, kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa nane na nusu Adhuhuri, idara imeandaa usafiri kwa washiriki bure.
Kwa maelezo zaidi fika ofisi zilizopo Karbala – mtaa wa Mulhaqu – barabara ya Hospitali ya Hussein – kituo cha Swidiqatu-Twahirah (a.s) cha harakati za wanawake – jirani na chuo cha Swahibu-Zamaan (a.f) ghorofa ya tatu.