Kitengo cha Dini kimeratibu semina ya kuwajengea uwezo watumishi wa shirika la Liwaaul-Aalamiyya

Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya, kimeandaa semina ya kuwajengea uwezo watumishi wa shirika la Liqaaul-Aalamiyya.

Mkufunzi wa semina Shekhe Daakhil Nuri amesema “Idara ya Dini chini ya kitengo, imeandaa semina ya kuwajendea uwezo watumishi wa shirika la Liwaaul-Aalamiyya, chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi ya kufanya semina za kidini kweye vitengo tofauti vya Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akaoingeza kuwa “Washiriki wa semina ni watumishi 30, imehusisha mada za Aqida, Hukumu za kisheria, vitenguzi vya swala pamoja na mambo mengine mengi ambayo mtumishi anatakiwa kuyajua”.

Akasema kuwa semina itadumu kwa muda wa siku tato, siku ya mwisho washiriki watapewa jaribio la kupima uwelewa wao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: