Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya, kimetoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru wa malalo ya Maimamu wawili Askariyaini (a.s) katika mji wa Samaraa, wakati wa kuomboleza kifo cha Imamu Ali Alhaadi (a.s).
Kiongozi wa idara ya maelekezo na msaada Shekhe Haidari Aaridhwi amesema “Kitengo kimehudumia mazuwaru kupitia maukibu waliyoweka karibu na Atabatu Askatiyya, kwa kushirikiana na mgahawa (mudhifu) wa Atabatu Abbasiyya, wamegawa milo mitatu ya chakula kwa mazuwaru kila siku, wamegawa zaidi ya sahani elfu 20 za chakula kikuu sambamba na ugawaji wa vyakula vidogo vidogo”.
Akaongeza kuwa “Kitengo kimeandaa sehemu ya kupumzika na kulala, yenye uwezo wa kuchukua watu 1500 wanaume na wanawake”.
Akafafanua kuwa “Kitego cha Dini kimefungua kituo cha kujibu maswali ya kisheria kwa mazuwaru”.






