Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini amepokea makundi ya watu wanaokuja kumpongeza kwa kuteuliwa tena kuendelea na jukumu la ukatibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya kwa muda wa miaka mingine mitatu.
Watu kutoka makundi tofauti ya jamii wamekuja Ataba tukufu kumpongeza katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya kwa kuteuliwa kuengelea na madaraka hayo, wamemuomba Mwenyezi Mungu amuwezeshe kuitumikia malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na mazuwaru wake.
Tamko la uongozi wa Wakfu-Shia linasema “Kutokana na kuafiki Marjaa-Dini mkuu Sayyid Ali Hussein Sistani tarehe 13 Rabiul-Aakhar1446h, na kuzingatia kifungu cha (4) tatu H, cha kanuni ya uongozi wa Wakfu-Shia namba (57) ya mwaka 2012, kulingana na maslahi ya utendaji, tumeamua kumteua Sayyid mustwafa Murtadhwa Abudi Aalu Dhiyaau-Dini kuwa katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa muda wa miaka mingine mitatu, kuanzia tarehe ya kuisha kwa muda wa kwanza”.
Akaongeza kuwa “Sayyid Mustwafa Murtadha Abudi Aalu Dhiyaau-Dini, anawajibika kumteua makamo wake na wajumbe watato wa kamati kuu watakaofanya kazi chini yake”.
Sayyid Aalu Dhiyaau-Dini aliteuliwa kuchukua nafasi hiyo mwanzoni mwa mwezi wa Januari mwaka 2022 akimrithi Muhandisi Muhammad Ashqar.
Kabla ya kuchaguliwa kuwa katibu mkuu alikuwa mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya tukufu, tangu aliposhika madaraka hayo ametembelea miradi mingi na kukagua huduma mbalimbali zinazotolewa kwa mazuwaru.
Aidha ameimarisha ushirikiano na Ataba zingine kwenye sekta tofauti, kwa lengo la kuboresha huduma kwa mazuwaru.
Uteuzi wa Sayyid Mustwafa umepokelewa kwa shangwe na watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wameonyesha furaha kubwa na kumtakia mafanikio mema katika utekelezaji wa majukumu yake.







