Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya kimeandaa program ya (Uwanja wa utamaduni) kwa wanafunzi wa shule za Dini (Kitakachofanywa kwa ajili ya Alla kitakua) katika mnasaba wa kuadhimisha mazazi ya Imamu Muhammad Aljawaad (a.s).
Program imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, iliyofuatiwa na muhadhara wenye anuani isemayo (Funguo za ridhaa na utulivu katika maisha) uliotolewa na Dokta Maryam Abdulhusein, ameeleza namna ya kupata utulivu kwa kumdhania vizuri Mwenyezi Mungu na kumtegemea.
Kulikuwa na kipengele kiitwacho “picha na maoni” kilicho ongozwa na Imani Maula, wanafunzi wamechambua picha na kutoa maoni yao kulingana na muonekano wa picha”.
Program ya (Uwanja wa utamaduni) inaonyesha mtazamo wa kituo cha utamaduni wa familia katika kujenga uwelewa wa kitamaduni kwa washiriki, na kuwafungamanisha na mafundisho ya Ahlulbait (a.s) kwa kukusanya faida za kielimu na maadhimisho ya matukio matukufu.


