Atabatu Abbasiyya imefanya mashindano ya kitamaduni katika kuadhimisha mazazi ya Imamu Ali (a.s)

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya, umetangaza kufanyika kwa shindano la kitamaduni katika kuadhimisha mazazi ya kiongozi wa waumini Imamu Ali (a.s).

Majina kumi ya washindi yatatangazwa siku ya Jumapili tarehe (26/1/2025m) kwenye jukwaa la Atabatu Abbasiyya, sharti la kupokea zawadi, mshindi anatakiwa awepo kwenye hafla ya Qur’ani itakayofanywa siku ya Jumanne (27 Rajabu 1446h) ndani ya haram tukufu katika kuadhimisha kupewa Utume kwa Mtume mtukufu (s.a.w.w) baada ya swala ya Magharibi na Ishaa.

Iwapo mshindi atapata udhuru wa kushindwa kuhudhuria, atatakiwa kwenda katika ofisi za wahasibu ndani ya siku zisizozidi nne (4) toka kutolewa kwa matokeo, akiwa na nyaraka zinazo mthibitisha (kitambulisho cha uraia au hati ya kusafiria)
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: