Kitengo cha maadhimishi na mawakibu Husseiniyya kinasimamia uratibu na usimamiaji wa matembezi ya mawakibu za kuomboleza.
Makamo rais wa kitengo Sayyid Kadhim Swalehe amesema “Mawakibu za kuomboleza zinaendelea kumiminika katika mji wa Karbala kutoka mikoa tofauti, zikiwa katika mazingira ya huzuni na majonzi kutokana na kuomboleza kifo cha Bibi Zainabu (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Mawakibu za kuomboleza zinaelekea katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kumpa pole, kisha kwenye malalo ya Imamu Hussein (a.s), kwa kupitia kwenye uwanja wa katikati ya harama mbili takatifu au kinyume chake”.
Kiongozi wa kikundi cha Zaidu Shahidi (a.s) Sayyid Hussein Hamza amesema “Watu wa Karbala katika siku kama huzi wamezowea kuomboleza kifo cha Bibi Zainabu (a.s) kwa kufanya mawakibu za uombolezaji”.
Akaongeza kuwa “Atabatu Abbasiyya imeturahisishia uombolezaji wa matukio ya Ahlulbait (a.s), kipitia kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya”.







