Idara ya Fatuma binti Asadi (a.s) kwa kushirikiana na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya imeomboleza kumbukumbu ya kifo cha Bibi Zainabu (a.s).
Kiongozi wa idara ya Fatuma binti Asadi (a.s) Bibi Fatuma Mussawi amesema “Ratiba ya (Manaahil Rawiyya) na (Fas-alu Ahla Dhikri) iliyofanywa siku ya Ijumaa ikiwa ni sehemu ya kukumbuka historia ya Bibi Zainabu (a.s) sambamba na kuomboleza kifo chake kwa kushirikiana na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake”.
Akaongeza kuwa “Mzungumzaji ameongea mambo mawili makuu katika maisha ya mtu na jamii, nayo ni uadilifu na wema, na jinsi Bibi Zainabu (a.s) alivyo pambika na sifa hizo tukufu”.
Akasema kuwa “Sambamba na kueleza somo la subira na msimamo, majlisi ikahitimishwa kwa kusoma Dua Faraj na Suratul-Faatihah kwa ajili ya kuwarehemu waumini”.
Atabatu Abbasiyya tukufu huadhimisha matukio yoto yanayohusu Ahlulbait (a.s) kwa lengo la kusambaza ujumbe wao na kuhuisha mwenendo wao mtukufu.


