Kongamano la Aqilah katika chuo kikuu cha Kirkuk limeshuhudia muhadhara kuhusu historia ya Bibi Zainabu (a.s) na msimamo wake pamoja na kaka yake Imamu Hussein (a.s).
kongamano limeandaliwa chini ya kauli mbiu isemayo (kujistiri na jihadi), likiwa ni sehemu ya mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel chini ya kitengo cha mahusiano katika Ataba tukufu, linafanywa kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Kirkuk katika kuomboleza kifo cha Bibi Zainabu (a.s).
muhadhara uliotolewa na Sayyid Qambar Mussawi umejikita katika kueleza historia ya Bibi Zainabu Alkubra (a.s) na msimamo wake alipokua pamoja na kaka yake Imamu Hussein (a.s), hususan katika kulinda familia yake baada ya tukio la Karbala.
Muhadhara umeeleza nafasi yake (a.s) katika uwanja wa tablighi na kutetea haki za Ahlulbait (a.s), namna alivyo simama kishujaa mbele ya watawala waovu na jinsi alivyo linda hijabu yake katika mazingira magumu.
Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya mikutano na makongamano mbalimbali kwenye vyuo vikuu vya Iraq katika kuadhimisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) na kuimarisha mafungamano ya wanafunzi na mwenendo mtukusu wa Ahlulbait (a.s),




