Kazi ya kushona vitambaa na kuandaa mabango imefanywa na idara ya ushonaji na kudarizi chini ya kitengo cha zawadi na nadhiri katika Ataba tukufu.
Mabango yamewekwa juu ya pambo la sega linaloelekea kwenye haram tukufu ya malalo ya Abulfadhil Abbasi na sehemu zinazozunguka eneo hilo, zimetumika aina maalum za gundi katika uwekaji wa mabango hayo.
Atabatu Abbasiyya huzingatia maombolezo ya kifo cha Imamu Mussa Alkadhim (a.s) kwa kuandaa ratiba kamili, inayo husisha ufanyaji wa majlisi na utoaji wa mihadhara, sambamba na kueleza nafasi yake katika kulinda ujumbe wa babu yake Mtume mtukufu (s.a.w.w).







