Atabatu Abbasiyya imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Alkadhim (a.s)

Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Mussa Alkadhim (a.s) ndani ya haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Mhadhiri wa majlisi Shekhe Muhammad Jasaam Shimri amesema “Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Mussa Alkadhim (a.s) ndani ya ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) iliyohudhuriwa na kundi kubwa la waumini”.

Akaongeza kuwa “Atabatu Abbasiyya huadhimisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) kutokana na umuhimu wa kusambaza fikra za Maimamu watakasifu (a.s).

Akaendelea kusema “Tunafanya hivyo kutokana na umuhimu mkubwa wa kunufaika na mafundisho mazuri yanayotokana na historia ya Maimamu watakasifu (a.s), yanayo wafundisha waumini jinsi ya kupambana na changamoto, hususan katika zama hizi ambazo kuna upotoshaji mkubwa unaofanya na baadhi ya vyombo vya habari kwa lengo la kupoteza vijana na jamii”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: