Atabatu Abbasiyya inaendelea kuomboleza kifo cha Imamu Alkadhim (a.s) kwa kufanya majlisi ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Mhadhiri wa majlisi Shekhe Swalahu Abudi ameongea mambo mengi, ikiwemo historia ya Imamu Alkadhim (a.s), na kipindi alichoishi na baba yake Imamu Jafari bun Muhammad Swadiq (a.s) na mambo yaliyotokea katika kipindi hicho.
Majlisi imeeleza mazingira magumu aliyopitia Imamu (a.s) na ukweli kuhusu kipindi alichokaa gerezani na jinsi alivyokua akifikisha mafundisho kwa wafuasi wake.
Atabatu Abbasiyya tukufu huhuisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) kwa lengo la kuiga mwenendo wao na kusambaza elimu yao.












