Kitengo cha kusimamia haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya, kimeweka mabango yanayoashiria furaha katika kuadhimisha mazazi ya miezi ya Muhammadiyya (a.s).
Kazi ya kushona mabango imefanywa na idara ya ushonaji na kudarizi chini ya kitengo cha zawadi na nadhiri katika Ataba tukufu.
Makamo rais wa kitengo hicho Sayyid Zainul-Aabidina Quraishi amesema “Watumishi wa kitengo cha kusimamia haram wameweka maua na mabango yaliyoandikwa maneno ya pongezi ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na milangoni, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha kuingia mwezi mtukufu wa Shabani na kumbukumbu ya kuzaliwa miezi ya Muhammadiyya (a.s).
Akaongeza kuwa “Kazi zilizofanywa na kitengo ni sehemu ya mkakati wa kamati kuu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Akabainisha kuwa “Mkakati unavipengele vingi, miongoni mwake ni maandalizi ya kongamano kuu katika kuadhimisha mazazi takatifu, litakalofanywa katika mlango wa qibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na mambo mengine yatakayofanywa sehemu mbalimbali chini ya usimamizi wa Ataba tukufu”.






