Watumishi wa kitengo cha kusimamia haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya, wametoa pongezi kwa mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Hussein bun Ali (a.s).
Malalo ya Abukfadhil Abbasi (a.s) imeshuhudia idadi kubwa ya waumini waliokuja kuhuisha tukio hilo adhim, mazingira ya ukumbi wa haram tukufu yamepambwa na muonekano wa shangwe na furaha kwa mazuwaru.
Tukio hili ni sehemu ya juhudi za Atabatu Abbasiyya ya kuimarisha misingi ya kiroho katika jamii na mazuwaru, sambamba na kujenga mapenzi na utiifu kwa Ahlulbait (a.s) kufuatia kuadhimisha matukio ya kidii kama haya.





