Atabatu Abbasiyya tukufu, imewapa zawadi washindi wa shindano la kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Ali bun Hussein Sajjaad (a.s).
Imefanya hivyo katika hafla iliyofanywa kwenye uwanja wa mlango wa Qibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wakati wa kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Sajjaad (a.s).
Washindi kumi wamekabidhiwa zawadi na mjumbe wa kamati kuu ya Ataba tukufu Dokta Abbasi Didah Mussawi na baadhi ya viongozi wengine, kwenye jukwaa la hafla ya maadhimisho.
Washindi waliopata udhuru wa kushindwa kufika kwenye hafla hiyo, wanatakiwa kwenda katika ofisi za wahasibu wa Atabatu Abbasiyya ndani ya muda usiozidi wiki mbili toka kutangazwa matokeo hayo, wakiwa na nyaraka zinazowathibitisha (kitambulisho cha uraia au hati ya kusafiria)




