Idara ya Ataba tukufu inaangalia maandalizi ya kitengo cha Maqaam ya ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani

Kamati ya uongozi wa Atabatu Abbasiyya na msimamizi wa kitengo cha Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) Sayyid Kadhim Abada, wamekagua maandalizi ya kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Mahadi (a.f).

Wamekagua sehemu za kutolea huduma na mkakati wa kupokea idadi kubwa ya mazuwaru inayotarajiwa katika siku za nusu ya mwezi wa Shabani, sambamba na mkakati wa kuongoza matembezi ya mazuwaru watakaokuja kwenye maqam tukufu.

Sayyid Abada akaelekeza huduma zinazotakiwa kutolewa na maandalizi ya kimkakati pamoja na kubainisha uhusiano wa vitengo tofauti wakati wa ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: