Mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya na mkuu wa shirika la Teknolojia ya kilimo cha kisasa na viwanda Khairul-Juud Sayyid Kadhim Abada amekagua shughuli za kilimo kinachofanywa na shirika.
Abada ametembelea shirika la Khairul-Juud ambalo lipo chini ya Ataba tukufu, amekutana na katibu mtendaji wa shirika Sayyid Maitham Bahadeli, ikiwa ni sehemu ya ratiba ya uongozi wa Ataba tukufu.
Ziara imehusisha kukagua mitambo ya kisasa inayotumiwa na shirika kwenye mambo mbalimbali pamoja na sekta ya kilimo cha kisasa.
Katika ziara hiyo wamesikiliza maelezo ya kina kuhusu kilimo cha nyanya, na kujadili vifaa vya kilimo na viwatilifu vinavyo hitajika katika kuboresha sekta hiyo.





