Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imefaya hafla ya (Anwaaru-Shaabaniyya) katika kuadhimisha kuzaliwa kwa miezi ya Muhammadiyya (a.s) katika wilaya ya Suuq-Shuyuukh mkoani Dhiqaar.
Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Dhiqaar imesimamia hafla hiyo kwa kushirikiana na mradi wa utamaduni wa vijana wa Iraq na msikiti wa Aali-Haidari hapo mkoani.
Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Ali Qassim Al’aamiri, ukafuata ujumbe wa makaribisho kutoka kwa Shekhe Muhammad Hassan Aali-Haidari, kisha ukafuata ujumbe elekezi kutoka kwa muwakilishi wa Marjaa-Dini mkuu Shekhe Hussein Aalu Yaasin.
Hafla imepambwa na qaswida na mashairi kutoka kwa Hassan Haji Akalah, Abbasi Abdusaadah, Fadhili Swabri, Hassan Alhajimi pamoja na tenzi za kuwasifu Ahlulbait (a.s) kutoka kikosi cha vijana cha Nuru.
Ikahitimishwa kwa kuwapa zawadi washiriki, ikiwa ni sehemu ya kuonyesha thamani ya kuadhimisha kumbukumbu ya watakasifu waliozaliwa katika mwezi wa Shabani.












