Idara inayosimamia haram imetoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru wa nusu ya mwezi wa Shabani

Watumishi wa idara inayosimamia haram ya Atabatu Abbasiyya wametoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wakati wa ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani.

Miongoni mwa huduma walizotoa ni: Kuongoza matembezi ya mazuwaru, kuteua milango ya kuingia na kutoka ndani ya haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Aidha wamepuliza marashi ndani ya haram tukufu, wameweka vitabu vya dua na ziara kwenye kabati za vitabu pamoja na huduma zingine nyingi.

Makundi ya waumini kutoka ndani na nje ya Iraq, yamefanya ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani mbele ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wamefanya kila wawezalo katika kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa mazuwaru wakati wa kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Mahadi (a.f).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: