Kuhitimisha ratiba ya mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq na nchi za kiislamu awamu ya nane

Atabatu Abbasiyya tukufu imehitimisha ratiba ya mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq na nchi za kiislamu kikosi cha (Mabinti wa Alkafeel) awamu ya nane.

Mahafali imesimamiwa na idara ya shule za Alkafeel za wasichana chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, na kauli mbiu isemayo (Kutokana na nuru ya Fatuma –a.s- tunaangaza dunia) kwa mwaka wa masomo 2023/2024.

Mahafali inazaidi ya washiriki 4000 kutoka Iraq na 170 kutoka vyuo vikuu vya nchi za kiislamu: Kawait, Baharain, Oman, Lebanon, Iran, Pakistan na Saudia.

Mahafali imepambwa na kiapo cha kuhitimu, ahadi ya utiifu kwa taifa na matembezi katika eneo la katikati ya Ataba mbili takatifu Husseiniyya na Abbasiyya, ikahitimishwa na ratiba ya jioni iliyo husisha ujume elekezi uliorekodiwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, pamoja na kipengele cha utamaduni, mashairi na tenzi.

Mahafali hiyo imeshuhudia kipengele cha kutoa zawadi kwa familia za mashahidi kama sehemu ya kuonyesha kuthamini kujitolea roho zao kwa ajili ya Iraq, na kuliwaza familia zao, sambamba na kuwapa zawadi baadhi ya wakufunzi wa vyuo vikuu vya Iraq kama sehemu ya kupongeza juhudi zao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: