Mkuu wa Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Karbala chini ya Majmaa amesema, “Majmaa-Ilmi imefanya hafla ya kukamilisha mradi wa msimu wa Qur’ani kwa wanafunzi wa kitengo cha tahfiidh katika Maahadi, imehusisha utoaji wa zawadi kwa washiriki”.
Akaongeza kuwa “Mradi huu ni sehemu ya kunufaika na likizo, kwa kurejea kusoma walicho hifadhi kwa makundi: (Juzuu 5, juzuu 10 na waliohifadhi Qur’ani yote”.
Akabainisha kuwa “Tumeweka ratiba maalum ya kujisomea katika kipindi hiki cha likizo, sambamba na kufanya semina na warsha za kujenga uwezo katika sekta ya kijamii, saikolojia, kusimama na kuanza, hukumu za usomaji, sauti na naghma”.


































