Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imetoa muhadhara elekezi kwa ugeni wa wanafunzi kutoka mji wa Mashhadi nchini Iran.
Mkuu wa maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Karbala chini ya Majmaa, Shekhe Jawadi Nasrawi amesema “Maahadi imepokea ugeni wa wanafuni wa Dini kutoka mji wa Mashhadi, wameambiwa harakati mbalimbali za Qur’ani”.
Akaongeza kuwa “Ugeni umeangalia harakati za maahadi katika sekta ya kuhifadhi, kusoma na kutafsiri Qur’ani sambamba na kuangalia vipaji vya wanafunzi wa idara ya tahfiidh”.
Akaendelea kusema “Ziara inalenga kufungua ushirikiano na kubadilishana uzowefu, nalo ni sehemu ya mkakati wa Maahadi katika kupokea wageni wa taasisi za kidini na Qur’ani kutoka ndani na nje ya Iraq”.










