Kituo cha utamaduni wa familia kimefanya program ya walezi wa shule za msingi za Baghdad

Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya program ya walezi wa shule za msingi katika mji mkuu wa Baghdad.

Program hilo imepambwa na muhadhara usemao (Kuamiliana kwenye mafanikio na mwanafunzi wa shule ya msingi: kumjenga na kumuongoza) imetolewa na Dokta Maryam Abdulhussein, ameeleza misingi ya kuwasiliana na wanafunzi na umuhimu wa kuongoza tabia zao, akataja mbinu zinazosaidia kutoa malezi bora darasani.

Program hii ni sehemu ya kuwajengea uwezo walezi wa shule za msini, ili waweze kujenga kizazi cha watu wanaojitambua na kujiamini kwa kufuata misingi tuliyofundishwa na Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: