Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya amekutana na ugeni wa taasisi ya Ain katika mji wa Karbala

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya, Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini amekutana na ugeni wa taasisi ya Ain katika mkoa wa Karbala.

Sayyid Dhiyaau-Dini amepongeza kazi zinazofanywa na taasisi hiyo, ya kulea mayatima kutoka mikoa tofauti ya Iraq, akasisitiza kuendelea kwa ushirikiano baina ya Ataba na taasisi ya Ain kwa ajili ya malengo ya kibinaadamu yanayonufaisha jamii.

Kiongozi wa tawi la taasisi katika mkoa wa Karbala, Sayyid Hassan Alawi amesema “Ziara hii ni sehemu ya kutoa shukrani kwa Atabatu Abbasiyya tukufu kutokana na ushirikiano wake mkubwa katika kuhudumia jamii”.

Kikao kikahitimishwa kwa kumkabidhi ngao katibu mkuu, kama sehemu ya kupongeza mchango wa Ataba tukufu katika kuisaidia taasisi ya Ain misaada ya kibinaadamu na kijamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: