Kamati ya kuhisha turathi katika Atabatu Abbasiyya imefanya semina ya kielimu katika somo la Fiqhi kwa wanafunzi na watafiti wa kidini.
Semina imeratibiwa na Maahadi ya turathi chini ya kamati, kufuatia kuingia mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Semina imejadili mada mbalimbali, ikiwemo; Fiqhi-Kalami, utambulisho wake, kuanza kwake, historia yake, aina zake, matawi yake, umuhimu wake, pamoja na itikadi ya kufuata kizazi cha Mtume, kutambua wanaojitenga na suna za Mtume na sababi za kujitenga.
Mtoa mada katika semina hiyo ni Sayyid Ali Shahristani, itadumu kwa muda wa siku tano, kuanzia siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Maahadi imeandaa ratiba kamili ya kuhuisha usiku za mwezi mtukufu wa Ramadhani yenye vipengele tofauti vya kitamaduni na kidini.




