Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Bibi Khadija (a.s) ndani ya ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Rais wa kitengo Shekhe Swalahu Karbalai amesema “Kitengo kimefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Bibi Khadija (a.s) ndani ya ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa lengo la kujikumbusha historia yake tukufu na msimamo wake katika kunusuru Uislamu”.
Akaongeza kuwa “Majlisi imejadili vipengele muhimu katika maisha yake, hususan baada ya kumfahamu Mtume Muhammad (s.a.w.w) na kuolewa nae, sambamba na kuelezea mazazi ya Bibi Zahara (a.s) mama wa Maimamu watakasifu (a.s).
Akaendelea kusema “Bibi Khadija ni kigezo chema kwa wanawake wa kiislamu, alifanya kila awezalo katika kumsaidia mume wake Mtume wa Mwenyezi Mungu (a.s.w.w), hakika alikuwa mke bora anatakiwa kuigwa na mabinti zetu”.
Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa mihadhara ya kidini kipindi chote cha mwezi mtukufu wa Ramadhani, ikiwa ni sehemu ya kuwajengea mazuwaru, uelewa wa Dini na mafundisho ya Ahlulbait (a.s).



