Kiongozi wa vitalu Sayyid Muhammad Harbi amesema “Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa hafla mbalimbali za kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Hassan Almujtaba (a.s) kwenye maeneo tofauti, likiwemo eneo la vitalu vya Alkafeel”.
Akaongeza kuwa “Hafla imepambwa na usomaji wa tenzi, qaswida na mashairi kutoka kwa waimbaji mahiri mbele ya familia za watu wa Karbala sambamba na utoaji wa zawadi za maua kwa wahudhuriaji”.
Akasema kuwa “Atabatu Abbasiyya huadhimisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s)”.





