Kituo cha utamaduni wa familia kimeandaa ratiba maalum kwa wanafunzi wa shule ya Jamana katika mji wa Karbala

Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya, kimeandaa ratiba maalum yenye anuani isemayo (msimu wa utamaduni) kwa wanafunzi wa shule ya Jamana katika mkoa wa Karbala.

Ratiba imefanywa kwa kushirikiana na idara ya mambo ya wanawake katika shule ya Tarbiyya iliyopo Karbala, kulikuwa na mihadhara miwili, muhadhara wa kwanza ulikuwa na anuani isemayo (hadhi ya mtu), umewasilishwa na Nabaa Haidari, ameongeo kuhusu umuhimu wa kuweka malengo katika kupata mafanikio, na upangiliaji wa muda na vipaombele.

Muhadhara wa pili ulikuwa na anuani isemayo (hatua za kuweka malengo), imewasilishwa na Bibi Adhraa Ahmadi, ameeleza umuhimu wa kuwa na malengo ndio hatua ya msingi ya kufanikiwa katika maisha.

Ratiba hii ni sehemu ya harakati za kimalezi zinazolenga kujenga vipaji vya wanafunzi na kupangilia maisha yao kimasomo na binafsi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: