Kamati kuu ya kuhuisha turathi imechapisha kitabu cha (Urithi) kilicho andikwa na Allamah Twaharani

Kamati kuu ya kuhuisha turathi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imechapisha kitabu cha (Urithi) kilicho andikwa na Allamah Mhakiki Shekhe Muhammad Haadi Twaharani.

Kitabu kimehakikiwa na Shekhe Abdul-Ilahi Shaibu Alqatwifi, Shekhe Ali Aqili Al-Ihsaai na kikapitiwa na kituo cha Shekhe Tusi cha tafiti na uhakiki chini ya kamati.

Muandishi wa kitabu kaeleza mambo mbalimbali ya urithi sambamba na kuweka dalili madhubuti, kaonyesha muhtasari bainifu wa kifiqhi na usulu.

Kitabu kina ufafanuzi wa kina kwa kutumia riwaya tukufu na tafiti za urithi.

Kitabu hiki ni miongoni mwa mfululizo wa tunzi za Allamah Twaharani, ambae amefanya kazi kubwa ya kielimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: