Waziri wa utamaduni katika serikali ya Iran amepongeza tawi la Atabatu Abbasiyya linaloshiriki kwenye maonyesho ya vitabu kimataifa jijini Tehran

Waziri wa utamaduni na mafundisho ya kiislamu nchini Iran, Sayyid Abbasi Swalehe, anepongeza tawi la Atabatu Abbasiyya linalo shiriki kwenye maonyesho ya vitabu kimataifa awamu ya thelathini na sita.

Ametoa pengezi hizo baada ya kutembelea tawi la Ataba tukufu na kuangalia machapisho yake ambayo ni zaidi ya 350.

Ameangalia aina za machapisho na malengo yake kifikra na kielimu, akapongeza ubora wake kielimu, hususan kitabu cha fatwa ya jihadi kifanya ya kujilinda, kinacho elezea fatwa iliyotolewa na Marjaa-Dini mkuu, akasema kuwa ni kitabu muhimu sana katika historia ya taifa la Iraq.

Maonyesho yanafanywa katika nchi ya Iran kuanzia tarehe 8 hadi 17 Mei kwa ushiriki wa nchi zaidi ya 70.

Ushiriki wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye maonyesho hayo, ni muendelezo wa ushiriki wake katika maonyesho ya kimataifa na kitaifa, kwa lengo la kuimarisha mawasiliano na kubadilishana uzowefu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: