Makundi ya mazuwaru yamehuisha usiku wa Ijumaa mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Mji wa Karbala hupokea idadi kubwa ya mazuwaru wanaokuja katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kuhuisha utiifu wao kwa Ahlulbait (a.s).
Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa mkakati maalum wa kutoa huduma unaohusisha sekta ya usalama, afya na mambo mengine, ikiwemo kuongoza matembezi ya mazuwaru mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).