Wahudumu wa idara ya Masayyid katika Atabatu Abbasiyya, wamehudumia mazuwaru katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) siku ya Arafa kupitia maukibu ya utoaji wa huduma.
Maukibu inatoa huduma mbalimbali kupitia maukibu iliyopo katika mlango wa qibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ikiwa ni pamoja na kugawa maji baridi ya kunywa na huduma zingine nyingi zinazotolewa ndani na nnje ya haram tukufu.
Vitengo vya Atabatu Abbasiyya vinafanya kila viwezalo katika kuhudumia mazuwaru wanaokuja Karbala, kuhuisha siku ya Arafa na sikukuu ya Idul-Adh-ha.