Maukibu ya kitengo cha Dini inahudumia waombolezaji katika kumbukumbu ya kuzikwa miili mitakatifu

Maukibu ya kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya, inahudumia mazuwaru wanaoshiriki kumbukumbu ya kuzikwa miili ya mashahidi wa Twafu (Karbala).

Maukibu imejengwa katika uwanja wa Ummul-Banina (a.s) kwa lengo la kuhudumia mazuwaru wanaokuja kwenye malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Miongoni mwa huduma zinazotolewa na maukibu hiyo ni kujibu maswali ya mazuwaru, kugawa maji, juisi na maziwa baridi, kwa lengo la kupoza koo kutokana na uwepo wa joto kali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: