Wanahabari wa Atabatu Abbasiyya wameanza kuripoti matembezi ya Arubaini kutoka Ra-asubishah kusini mwa Iraq

Kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya kimeanza kuripoti matembezi ya ziara ya Arubaini kutoka mji wa Ra-asubishah uliopo kusini mwa Iraq katika mkoa wa Basra, ukiwa ndio mwanzo wa matembezi ya Arubaini ambayo huhudhuriwa na mamilioni ya watu kuelekea katika mji wa Karbala.

Wahudumu wa kitengo huanza kuripoti matembezi hayo kutoka kituo cha kwanza kabisa katika mkoa wa Basra hadi itakapofika misafara hiyo katika mji wa Karbala, kwa lengo la kuthibitisha tukio hilo na kufikisha ujumbe duniani.

Kazi hiyo hufanywa chini ya utaratibu maalum uliowekwa na kitengo, unahusisha picha, sauti na habari sambamba na kufanya matangazo ya moja kwa moja (mubashara) kutoka katika misafara, uombolezaji, huduma zinazotolewa kwa mazuwaru kwa njia bora inayo onyesha ukubwa wa tukio hilo.

Jambo hilo linaonyesha namna Atabatu Abbasiyya inavyojali utoaji wa habari za mawakibu na matukio ya kidini yanayohusu Ahlulbait (a.s) kwa kutoa huduma ya habari inayoendana na malengo ya tukio.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: