Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, imekamilisha matembezi ya kuomboleza kifo cha Bibi Ruqayya (a.s) kwa kufanya majlisi ndani ya malalo ya Imamu Hussein (a.s).
Kiongozi wa idara Bibi Taghrida Tamimi amesema “Matembezi ya kuomboleza kifo cha Bibi Ruqayya (a.s) hufanywa kila mwaka mwezi tano Safar sambamba na kuangazia matatizo waliyopata watoto katika tukio la Karbala”.
Akasema kuwa “Matembezi ya mwaka huu yamekua na ushiriki mkubwa kutoka kwa tabaka tofauti za wanawake wa Ataba tukufu na wanafunzi, washiriki wamekua zaidi ya 1000 na wamehitimisha matembezi kwa kufanya majlisi ya kuomboleza”.









