Sardabu ya Ummul-Banina (a.s) ni moja ya vituo vikuu vinachopokea mazuwaru wa kike, imejengwa kwa ubora mkubwa, inanjia za dharura na vifaa vya zimamoto kwa lengo la kuhakikisha usalama wa watu wanaokaa hapo ndani.
Sardabu hiyo inavituo vya Dini, malezi na maelekezo, shughuli zote zinasimamiwa na wanawake kutoka idara tofauti za Atabatu Abbasiyya, huduma zinaendana na ukubwa wa ziara pamoja na idadi ya mazuwaru ambayo huongezeka kila mwaka.
Ufunguzi wa Sardabu hiyo ni sehemu ya maandalizi yanayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika kuhudumia mazuwaru na kuimarisha athari ya ziara hii kiimani kuelekea kumbukumbu ya kifo cha bwana wa mashahidi (a.s).







