Kitengo cha habari na utamaduni kimesema: tuligawa sahani za chakula laki moja na elfu kumi wakati wa ziara ya Arubaini

Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kiligawa zaidi ya sahani za chakula 110,000 wakati wa ziara ya Arubaini.

Rais wa kitengo Sayyid Aqiil Yasiri amesema: “Kupitia mkakati wa kuhudumia zuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), kitengo kilikuwa na mawakibu sita na kimegawa zaidi ya sahani za chakula 110,000 kwa zuwaru waliokuwa wanaelekea kwenye mji wa Karbala”.

Akaongeza kuwa “Watumishi wa kitengo wamegawa maji grasi 514,000, juisi 45000, mifuko ya barafu 38000, chai vikombo 45000, kilo 400 za matunda pamoja na huduma zingine mbalimbali kutokana na mahitaji ya zuwaru”.

Kitengo kilichagua sehemu nzuri za kuweka mawakibu za kutoa huduma kwa mazuwaru ndani na nje ya mji wa Karbala, kwa lengo la kuhudumia zuwaru wengi zaidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: