Watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya wameomboleza kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s) kupitia maukibu ya pamoja.
Maukibu imehudhuriwa na wajumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya Sayyid Kadhim Abadah, Sayyid Muhammad Ashqar na baadhi ya wahudumu wa Ataba mbili tukufu.
Mkuu wa majengo ya Abbasi (a.s) ya makazi chini ya Atabatu Abbasiyya Sayyid Haidari Majhuul amesema: “Wahudumu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya hufanya majlisi ya kuomboleza kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s) kupitia maukibu ya pamoja huku wakiimba qaswida na tenzi za kuomboleza”.
Akaongeza kuwa “Maukibu imefanya matembezi kuanzia malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ikapita kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, ikaenda hadi katika malalo ya Imamu Hussein (a.s) kumpa pole, aidha waombolezaji wameimba qaswida na tenzi zilizoamsha hisia za huzuni na majonzi katika nyoyo za waumini”.
Wahudumu wa Ataba mbili tukufu huomboleza kumbukumbu za vifo vya Maimamu wa Ahlulbait (a.s) kwa kufanya maukibu ya pamoja.












