Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, amesisitiza umuhimu wa kutunza kumbukumbu za matukio ya Iraq kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Ameongea hayo alipompokea rais wa taasisi ya utunzaji wa kumbukumbu Alwaafi, Sayyid Ahmadi Swadiq na wajumbe aliofuatana nao, akasikiliza maelezo ya kina kuhusu kitabu cha wafungwa wa kisiasa kinacho andikwa na taasisi hiyo.
Swadiq akasema: Wajumbe wa taasisi ya Alwaafi wamekutana na Muheshimiwa Sayyid Swafi na kuongea taarifa za hivi karibuni kuhusu kitabu cha wafungwa wa kisiasa na kumthibitishia Muheshimiwa mambo yanayohusu utawala wa kidikteta wa chama cha Baathi, ukizingatia kuwa yeye ni mmoja wa wafungwa wa kisiasa katika miongo hiyo ya giza, Muheshimiwa amesisitiza umuhimu wa kutunza kumbukumbu za matukio ya Iraq kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Akaongeza kuwa “Maelezo yote yamesajiliwa kwa ajili ya kuongezwa kwenye kitabu cha wafungwa wa kisiasa, sambamba na kutunza taarifa za picha za video katika taasisi”.

