Kuanza mwaka mpya wa masomo.. Chuo kikuu cha Al-Ameed kimeanza mwaka mpya wa masomo kwa kusaidia watoto yatima na wenye mazingira magumu

Kitengo cha harakati za wanafunzi katika chuo kikuu cha Al-Ameed, kimeanza kutoa misaada kwa watoto yatima na wenye mazingira mahumu, kufuatia kuanza mwaka mpya wa masomo.

Harakati hiyo imeratibiwa na idara ya kazi za kujitolea kwa kushirikiana na vitivo vyake, wanagawa mabeji ya shule na vifaa vya lazima kwa mayatima na wenye mazingira magumu, kwa ushiriki wa ugeni uliohusisha idadi kubwa ya viongozi wa idara za chuo na watumishi wake.

Kazi hiyo inatokana na maelekezo ya wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu, yenye lengo la kushajihisha wanafunzi kuendelea na masomo na kupunguza mzigo kwa familia zao sambamba na kujenga moyo wa kusaidiana katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: