Mji wa kitalii wa Firdausi chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, umeandaa zaidi ya vikao vya kifamilia 40 bure kwa watu wanaotembelea sehemu hiyo.
Kiongozi wa sehemu za kufanyia vikao, Sayyid Rajabu Kadhim Naif amesema “Mji wa kitalii wa Firdausi umefanya zaidi ya vikao 40 vya kifamilia bure, sehemu za kufanyia vikao vimewekwa mahitaji yote ya lazima na zimeandaliwa kupokea wanafamilia katika mji huo”.
Akaongeza kuwa “Watumishi wetu wanafanya kazi muda wote, wanasafisha na kuratibu sehemu za vikao kila siku, ili kuweka mazingira mazuri kwa wanafamilia”.
Mji unasehemu tulivu za kupumzika, kuna bustani zenye ndege na maua mazuri, kuna bwawa mbili zenye boti za kuvulia samaki, kuna sehemu za michezo, migahawa na maporomoko ya maji.






