Mji wa Firdausi chini ya Atabatu Abbasiyya unatoa huduma za afya bure kwa familia za kiiraq zinazotembelea eneo hilo.
Kiongozi wa idara ya madaktari katika mji huo Sayyid Muhandi Hashim Sharifu amesema “Mji wa Firdausi unatoa huduma mbalimbali kwa familia zinazotembelea mji huo, ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za afya bure”.
Akaongeza kuwa “Huduma ya afya inatolewa na madaktari bobezi katika kazi hiyo, wakiwa na gari ya wagonjwa ambayo ikotayali kupeleka mgonjwa katika hospitali ya karibu”.
Mji wa Firdausi unamaeneo tofauti ya kitalii, unabustani za ndege na mauwa, bwawa mbili, moja kwa ajili ya shughuli za kilimo na linguine uvuvi wa samaki, sehemu za michezo, sehemu za migahawa na maporomoko ya maji.



