Kamati ya ratiba za Atabatu Abbasiyya imefanya warsha yenye anuani isemayo (Habari mficho) kwa ushiriki wa kundi kubwa la watumishi.
Warsha imesimamiwa na kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Ataba tukufu.
Mkufunzi wa warsha Sayyid Haidari Hariri amesema: “Warsha imejikita katika kueleza maudhui za habari na jumbe fiche, kwani jumbe hizo ni siraha ya habari mficho, sambamba na njia za kupambana na upotoshaji wa taarifa”.
Akaongeza kuwa “Warsha inalenga kuimarisha sekta ya habari kwa watumishi, na kuwahimiza kutegemea habari rasmi zenye uhakika, ikiwa ni pamoja na mbinu za kuchuja habari zinazosambazwa na mitandao ya kijamii”.



